×

Jordan Peterson ni profesa, mwanasaikolojia wa kimatibabu na msomi.

Jordan Peterson ni profesa, mwanasaikolojia wa kimatibabu na msomi.

Jordan alishinda jukwaa la dunia shukrani kwa utafiti wake katika saikolojia na falsafa. Video na mihadhara za Profesa Peterson zimetazamwa zaidi ya mara milioni 600, na midahalo na mahojiano yake na watu maarufu kama wale Joe Rogan, Matthew McConaughey, na Sam Harris ni maarufu sana.


Akili na uwezo wake wa kuunganisha mada mbalimbali zinazopingana kama vile uwajibikaji wa kibinafsi, maadili ya maisha, dini, na maana ya maisha zinamwadhimisha sana. Kitabu cha Dk Peterson "12 rules for life. Antidote to Chaos" kimekuwa na mafanikio makubwa. Hicho ndicho kitabu kilichouzwa sana nchini Kanada, Marekani na Uingereza. Karibu nakala milioni 6 zimeuzwa ulimwenguni kote. Kitabu hicho kiliwahimiza maelfu ya watu kuleta mpangilio katika maisha yao na kuboresha ulimwengu kuanzia na wao wenyewe. Wakati wa ziara ya kuendeleza mauzaji ya vitabu, Jordan Peterson alitembelea miji 130 akikusanya wasikilizaji hadi watu 25000.

Kitabu cha kwanza cha Dk Peterson "Maps of the Meaning. The Architecture of Belief" ,kinasemea kuhusu imani na hekaya. Maandiko hayo yamebadilisha mtazamo na saikolojia ya dini za watu wengi.

Jordan kwa sasa anafanya kazi na kitabu chake kipya kiitwacho "Beyond Order: 12 More Rules for Life" , kitabu hicho kitatolewa ulimwenguni mwezi Machi 2021.

Kipaji na ujasiri za Jordan Peterson katika taarifa zake zimemletea umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii: amepata zaidi ya wafuasi milioni 8 duniani. Idhaa yake ya YouTube ni maarufu sana kati ya wafuasi na wakosoaji wake hasa kwa majibu ya Jordan kwa masuala yenye utata yaani ya siasa na jinsia na mahojiano na watu maarufu.

Jordan Peterson pia ni mtungaji wa podikasti maarufu na kozi ya mtandao iitwayo "Utu" ambayo inasaidia kuelewa vizuri utu na nafsi, kutoa vipaumbele maishani na kuendeleza shughuli na maisha ya faragha.

01 /

Video maarufu Video maarufu

Vorstellungsvideo

Video ya kwanza ya Jordan, inayo maelezo juu ya maisha yake na juu ya shughuli zake za kitaaluma na ubunifu

01 / 03

Kitabu kipya “Beyond order; 12 More Rules for Life”

Taarifa juu ya kitabu

Katika wakati mgumu, Jordan Peterson huunda sheria mpya 12 za maisha. Sheria hizo ni ukweli kulingana na miongo kadhaa ya utafiti wa kisayansi na uzoefu wa kibinafsi na wa kitaalam ambao unaweza kumsaidia msomaji. Wakati wa kukosekana kwa utulivu na kuongezeka kwa shinikizo la kisaikolojia, anatukumbusha kuwa kuna vyanzo ambavyo vinaweza kutupatia nguvu.

Mawazo yaliyokopwa kutoka saikolojia, falsafa, hadithi kuu za dunia, na historia za wanadamu zimeundwa kuwa kanuni mpya kumi na mbili ambazo zinaweza kuongoza wasomaji maisha ya kuthubutu, halisi na yenye maana. Kitabu kitasaidia msomaji kuboresha hali ya maisha, kupata motisha ya kufikia malengo yao, na kukabiliana na shida za mahusiano.

Sheria za maisha